IDARA YA BIASHARA NA MASOKO

UTANGULIZI

Idara ya biashara na ukuzaji masoko ni miongoni mwa idara mama zilizo chini ya Wizara ya Biashara na Viwanda Zanzibar.

Idara hii ni inaongozwa na sheria ya biashara ya nam 14 ya mwaka 2013 “The Zanzibar Trading Act No 14 of 2013”.

Idara hii kwa ujumla wake husimamia na kutekeleza sheria na sera zinazohusiana na biashara Zanzibar pamoja na kuhamasisha (kukuza) masoko ya ndani, kikanda na kimataifa.

Idara imeweza kufuatilia kwa karibu na kuhakikisha inaimarisha hali ya biashara Zanzibar.

Kumekuwa na ongezeko la bidhaa zinaoingia ndani ya nchi na kuongezeka kwa thamani kwa asilimia 68 kutoka bidhaa zenye thamani ya TZS bilioni 211.42 mwaka 2017 na kufikia TZS bilioni 355.85 mwaka 2018 huku mazingira ya kufanya biashara yamewekwa kuwa rafiki kwa waekezaji nchini.

KAZI ZA IDARA YA BIASHARA.

Idara ya biashara ina kazi zifuatazo kama zilivyoanishwa katika sheria mama ya biashara.

1. Kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya uundwaji, uendelezaji, usimamizi na utekelezaji wa sera za biashara na mikakati yake.
2.  Kutekeleza sheria na sera zinazohusiana na biashara Zanzibar.
3.  Kuhamasisha (kukuza) masoko ya ndani, ya kikanda na kimataifa.
4.  Kushirikiana na Taasisi nyengine katika masuala ya uzalishaji, uingizaji wa bidhaa kutoka nje na kutoa huduma.
5.  Kutafuta na kutoa taarifa za biashara zinazohusiana na mauzo, manunuzi ya mahitaji ya biadhaa mbali mbali kwa watumiaji pamoja na kuishauri Serikali, jumuiya za biashara pamoja na wafanyabiashara mmoja mmoja. .
6.  Kusimamia biashara za ndani, za kikanda na kimataifa na kutoa elimu na uwelewa unaofaa katika ukuzaji wa Biashara.
7.  Kuweka mazingira bora (mazuri) kwa kuanzisha Public Private Partneship hususan katika mipango, utekelezaji na usimamizi wa agro processing initiatives kwa bidhaa za kilimo.
8.  Kukuza business interprises zikiwemo wajasiriamali wadogo na wakati (SMEs) na kuhimiza ukuaji na uongezaji wa faida katika mauzo ya biashara za ndani, kikanda na kimataifa.
9.  Kufuatilia na kutathmini mfumo wa biashara na ufafanuzi wake.
10.  Kufanya tafiti za masoko, survey na ufuatiliaji.
11.  Kuratibu na kushiriki maonesho ya biashara, misafara ya biashara pamoja na matamasha ya biashara ya ndani na nje..
12.  Kuweka njia au mfumo muafaka kwa wazanzibari kuchukua nafasi katika biashara za kimataifa na kushiriki kikamilifu katika maonesho ya biashara ya kimataifa.
13.  Kuratibu na kushiriki maonesho na matamasha ya kimataifa ya biashara.
14.  Kutayarisha na kutoa ripoti ya mwaka ya biashara.

BAADHI YA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA YA BIASHARA NA MASOKO.

1.  Utoaji wa vibali kwa wafanyabiashara.
2.  Kupata taarifa sahihi ya bei ya bidhaa zinazodhibitiwa na serikali.
3.  Kuelewa kipimo halisi kinachokubaliwa na serikali.
4.  Kuelewa hali ya Biashara ya Zanzibar.
5.  Kuelewa namna ya hatua za kuanzisha biashara Zanzibar.
6.  Kkuelewa ratiba ya matamasha Zanzibar na namna ya kuweza kushiriki.
7.  Kutoa elimu kwa wajasiriamali kuhusu uendeshaji biashara.